song lyrics / Ambwene Mwasongwe / Ombi Langu lyrics  | FRen Français

Ombi Langu lyrics

Performer Ambwene Mwasongwe

Ombi Langu song lyrics by Ambwene Mwasongwe official

Ombi Langu is a song in Swahili

Huwaambia moyo
Ntakulinda
Maana najua kwamba kuna chemichemi
Ntakujengea boma uwe salama
Adui akija asikuweze
Usiruhusu maneno yakuvuruge
Usiruhusu hasira ikae kwako
Namuweka mlinzi awe ngome yako
Akupiganie ubaki salama

Bwana naomba utete nao wale
Wanaoteta nami
Naomba upigane na adui zangu wote
Mimi sitaki kubishana nao
Sitaki kupambana nao
Nisije nikakosea wakanilaumu
Maana wameshavuta upinde
Wapo kwenye mangojeo yao
Wamenuna wamekunja sura wana hasira nami
Kinachowafanya wasinidhuru ni kwamba hawajapata sababu
Wanahesabu hatua zangu nikosee waninase
Usiache mguu usogezwe unase kwenye mitego yao
Weka mngozeji kinywani mwangu anilinde nisiropoke

Heeeeeee
Hili ni ombi langu kwako
Mungu akukumbuke na wewe
Katembee na wewe ( Katembee na wewe )
Katembee na wewe ( Atakuwa mboni zangu akulinde )
Moyo wangu ( Wewe ni wimbo wangu )
Wewe ni bwana wangu ( Tena dawa ya moyoni mwangu )
Wewe u fahari yangu ( Ufahari yangu )
Wewe u ukuta wangu
Wewe u thamani yangu (Atakuwa mboni zangu akulinde)
Wewe u mwaminifu wangu

Bwana wewe unaweza (Aaaaaaaa)
Wewe ni Mungu uliye hai (Aaaaaaaa)
Wewe ni mfalme wa ajabu
Wewe unayeponya mioyo
Halleluya

Nifanye kama Yusufu
Uliyemwona mwota ndoto ukambariki
Wewe ulimwona waziri mkuu
Tofauti na wanadamu
Wakamtazama vingine walivyoweza
Baba yake alimwona mpelelezi awapeleleze ndugu zake
Ndugu zake walimwona ni mbeya wakamtupa shimoni
Wamidiani wakamwona biashara wakamuuza kwa Potifa
Mkewe Potifa kamtamani akamwona kijana mzuri
Wafungwa wenzake wakamsahau wakifikiri ni mwarifu
Wewe uliona ndoto ndani yake ukamfanya waziri mkuu
Na mimi nifanye kama Yusufu

Hili ni ombi langu kwako
Mungu akukumbuke na wewe
Katembee na wewe ( Katembee na wewe )
Katembee na wewe ( Atakuwa mboni zangu akulinde )
Moyo wangu ( Wewe ni wimbo wangu )
Wewe ni bwana wangu ( Tena dawa ya moyoni mwangu )
Wewe u fahari yangu ( Ufahari yangu)
Wewe u ukuta wangu
Wewe u thamani yangu (Atakuwa mboni zangu akulinde)
Wewe u mwaminifu wangu

Bwana wewe unaweza (Aaaaaaaa)
Wewe ni Mungu uliye hai (Aaaaaaaa)
Wewe ni mfalme wa ajabu
Wewe unayeponya mioyo

Wewe ni kisima kwako nitachota hekima
Kwako nitachota baraka
Kwako nitachota wema
Kwako nitachota ukuu
Kwakoo ooh, kwako nitajifunza
Kwako nitaburudika
Aaaaaah Aaaaah Aaaah Aaaah
Lyrics copyright : legal lyrics licensed by Lyricfind.
No unauthorized reproduction of lyric.

Comments for Ombi Langu lyrics

Name/Nickname
Comment
Copyright © 2004-2024 NET VADOR - All rights reserved. www.paroles-musique.com/eng/
Member login

Log in or create an account...

Forgot your password ?
OR
REGISTER
Select in the following order :
1| symbol at the bottom of the television
2| symbol to the left of magnifying glass
3| symbol at the top of the cross
grid grid grid
grid grid grid
grid grid grid