song lyrics / Ambwene Mwasongwe / Watoto Yatima lyrics  | FRen Français

Watoto Yatima lyrics

Performer Ambwene Mwasongwe

Watoto Yatima song lyrics by Ambwene Mwasongwe official

Watoto Yatima is a song in Swahili

Ilitokea hawakupenda
Ndio mzunguko wa maisha
Na kama lingekuwa fungu, wasingechagua
Wanahangaika wanateseka wanapata shida hawana tumaini
Wameshaachwa wako peke yao
Mungu watazame kama Baba yao
Wanakutegemea wewe, wanakutazama Bwana

Kilio wanacholia wanalilia moyoni
Maana hata wakilia nani atawafariji
Mungu uwasaidie uwatie moyo, mzigo uwe mwepesi

Jamii imewasahau wanahangaika hata wakiombaomba wanawafukuza
Wengine wanawatukana kuwaita chokoraa Mungu uwakumbuke
Mungu uwakumbuke

Wakiachwa peke yao ubaki nao
Kaa pamoja nao kwenye baridi Kali
Kavifunge vidonda vya mioyo yao
Kazibe pengo lililo mioyoni mwao, wakumbushe wewe ni Baba na Mama yao

Ayayayah una macho huoni na hata ukiona huoni umuhimu

Jifanye kama umekufa uko kuzima sasa inua macho yako tazama duniani
Watazame wanao wanavyoteseka wanadhurumiwa wananyanyasika

Sasa nyosha mkono wako, uwape chakula
Nenda kawatafutie vya kujifunikaaaa
Unagundua hauwezi maana hauna mwili
Tena hawakuoni, maana ulishakufa

Sasa unawafanya Nini watoto wa marehemu
Mbona unawadhurumu Mali za wazazi waoooo sivyo walivyokuachia ili uwanyanyaseee
Usiwatende ubaya ili usije kutendewa

Hivi una uhakika gani kama ukiondoka utamwachia nani watoto wakooo
Je! Wakija kuwatenda kama utendavyo wewe utajisikiaje?
Je! Hayo utayapenda?

Ayayayayyaah hali zao ni mbaya
Ayayayayyaah hali zao ni mbaya

Tazama walivyopauka wa kwako wanatakata
Tena watupa chakula wao hawana
Wanatamani Baba angekuwepo
Mama angekuwepo wasingepata shida
Hawaelewi Nini kimewatokea
Wanjiona wana mikosi jamii imewasahau
Tuwahurumieni Hawa
Tuwaonyeshe upendo wetu

Wengine kwa kujitetea wakaangukia pabaya
Wamefuata mikumbo wako pabaya
Wengine wametenganishwa na wadogo zao
Wengine wako jela lakini tatizo Nini?
Walijaribu kuokoa maisha yao
Wakaenda kuiba
Wengine wanachomwa moto
Tunawalaumu Bado
Kumbe tatizo tumewasahau

Wananenewa maneno makali
Wanasimangwa Hadi wanauguaaaaaa
Ila wafanyaje wanajikaza
Hawana pa kwenda wanavumilia
Lyrics copyright : legal lyrics licensed by Lyricfind.
No unauthorized reproduction of lyric.

Comments for Watoto Yatima lyrics

Name/Nickname
Comment
Copyright © 2004-2024 NET VADOR - All rights reserved. www.paroles-musique.com/eng/
Member login

Log in or create an account...

Forgot your password ?
OR
REGISTER
Select in the following order :
1| symbol at the bottom of the house
2| symbol to the right of the star
3| symbol at the bottom of the clock
grid grid grid
grid grid grid
grid grid grid