song lyrics / Ambwene Mwasongwe / Ndoa lyrics  | FRen Français

Ndoa lyrics

Performer Ambwene Mwasongwe

Ndoa song lyrics by Ambwene Mwasongwe official

Ndoa is a song in Swahili

Mlilelewa na wazazi
Sasa mmekua
Ndio maana mmeamua, kuanza maisha yenu.
Mmeaacha baba na mama, kuwa mwili mmoja
Ndoa yenu ni takatifu, mtu asiwatenge
Bila shaka mmejifunza, mambo mbali mbali
Japokua mmepitia vipindi tofauti.
Katika yote hayo mshukuruni Mungu
Katika yote hayo mshukuruni Mungu
Kwa kua amewafikisha hapa mlipo
Kwa kua amewafikisha hapa mlipo

Safari yenu ya ndoa, mmeianza kwa imani
Ndio maana mwategemea, matokeo mazuri.
Yale mtakayotatua mshukuruni Mungu
Na yatakayowashinda mlilieni pamoja
Imani yenu yote iwekeni kwa Mungu
Msiweke katika vitu, shetani asije ona
Akipiga hivyo vitu imani yenu itayumba
Imani yenu ikiyumba nanyi mtayumba

Na ndoa yenu nayo itayumba
Na ndoa yenu nayo itayumba

Tunawaombea muende mkaanze maisha
Mungu wenu awalinde
Pingu ziwakubali
Neema ikawafunike
Bwana akawe mwalimu wenu
Mungu wenu akawe mshauri wenu

Ndoa ni kama kama jua lenye mwangaza mwanana
Kila lichomozapo wengi hulifurahia
watu makundi makundi hulisifia sana
Jua hili jua zuri lina faida kwa afya
Ila jua lilelile likifika mchana,
wengi hulalamika na kulikimbia
Joto likiwazidia wananung'unika
Joto likiwazidia wananung'unika
Wanasahau walilisifia asubuhi
Wanasahau walilisifia asubuhi

Jua likifika jioni, faraja hurejea tena
Ila bahati mbaya, jua laenda kuzama
Hapo sifa za asubuhi huanza kusikika upya
walovumilia mchana hula matunda yake
Ila tunawaombea Mungu awatetee
Mtakapofika mchana mkavumiliane
Joto likiwazidia, mkasameheane
Msilipize kisasi, msije kujidhuru.
Mkakumbuke jioni ya amani yaja
Mkakumbuke jioni ya amani yaja

Kama kuna jema lolote, msisite kulifanya.
Na neno la msamaha, msilicheleweshe
Mkaishi maisha yenu, msiige ya wengine
Epukeni mazoea, yanaleta kiburi
Tena maneno mabaya, uharibu tabia
Kamwe msije thubutu, kuyatunza moyoni.
Ndoa ni kipindi cha mwisho, cha maisha ya watu
Kitumieni vizuri, kwa kua ni kifupi
Maana hamjui lini kifo kitawatenga
Maana hamjui lini kifo kitawatenga

Mtendee wema mwenzako, kadiri utakavyoweza
Moyo unaweza kataa, ila jilazimishe
Kama ukitenda wema, huna utakachopoteza
Mtendee akiwa hai, macho yake yanaona
wengi wanajilaumu, kua walikosea
wakati wa kutenda wema wao waliumiza
Mungu akawatenganisha hawaishi pamoja
Wanatamani watende wema ila walichelewa
Maana wenzao hawapo tena
Maana wenzao hawapo tena

Mmeugusa moyo wa Mungu kwa kutimiza agano lake
Lyrics copyright : legal lyrics licensed by Lyricfind.
No unauthorized reproduction of lyric.

Comments for Ndoa lyrics

Name/Nickname
Comment
Copyright © 2004-2024 NET VADOR - All rights reserved. www.paroles-musique.com/eng/
Member login

Log in or create an account...

Forgot your password ?
OR
REGISTER
Select in the following order :
1| symbol to the right of the clock
2| symbol to the right of the television
3| symbol at the bottom of the thumbs up
grid grid grid
grid grid grid
grid grid grid