song lyrics / Rose Muhando / Kitimutimu lyrics  | FRen Français

Kitimutimu lyrics

Performer Rose Muhando

Kitimutimu song lyrics by Rose Muhando official

Kitimutimu is a song in Swahili

Nawauliza ninyi sasa mnaojikweza,
Hivi kweli mnajua ni nini mwisho mwisho wa maisha yenu?
Mnakula, mnakunywa lakini mbona hamfikirii?
Majigambo na dharau mi ubatili mtupu
Nawauliza ninyi sasa mnaojikweza,
Hivi kweli mnajua ni nini mwisho mwisho wa maisha yenu?
Mnakula, mnakunywa lakini mbona hamfikirii?
Majigambo ... na dharau ni ubatili mtupu!

Mwawadharau masikini wasiojiweza;
Neno lake Bwana Mungu ni upuuzi kwenu;
Mwawadharau Wahubiri wanapohubiri;
Injili yake Bwana Mungu ni upuuzi kwenu
Eti!
Mwajidanganya mwasema ponda mali
Kufa kwaja mmebobea kwenye dhambi kama wapumbavu
Vipofu msioijua njia mnayoiendea
Sasa geukeni!

Poleni kwenu sasa kwa kuwa mmehubiriwa
(Furaha) Furaha mliyo nayo itageuka msiba kwenu
(Chakula) Chakula cha anasa kitageuka mwamba wenu
(Sekese) Sekeseke kwa matajiri mwajipata mwalipwa pesa zenu
Poleni kwenu sasa kwa kuwa mmehubiriwa
(Furaha) Furaha mliyo nayo itageuka msiba kwenu
(Chakula) Chakula cha anasa kitageuka mwamba wenu
(Sekese) Sekeseke kwa matajiri mwajipata mwalipwa pesa zenu
(Visambutu)Kisambu kwa wake zenu wa mashabiki jinsi tabia Eeeeh

Walikuwepo matajari kama wewe
Wametoweka
Ni wazuri sana(ila sasa) lakini wako wapi sasa
Hawako tena
Walikuwepo una wasomi kama wewe
Wametoweka
Ni wazuri sana(ila sasa) lakini wako wapi sasa
Hawako tena
Kilikuwepo na warembo kama wewe
Walitoweka
Ni wazuri sana (ila sasa) lakini wako wapi sasa
Hawako tena
Walikuwepo kwa waimbaji kama mimi Rose
Wametoweka
Ni wazuri sana (ila sasa) lakini wako wapi leo

Hawako tena
Lakini Yesu kwa huruma anakubembeleza Yesu eh
Yesu yupo msalabani alisema njooni kwangu
Nitawasamehe dhambi
Nitabeba mizigo yenu
Ogopa kitimutimu
Siku yakuja kuuliwa
Yesu yupo msalabani
Anasema njooni kwangu
Nitawasamehe dhambi
Nitabeba mizigo yenu
Ogopa kitimutimu
Siku yakuja kuuliwa
Kasheeshe kwa watakaobaki kwenye viti kuu

Dunia hii isikudanganye Mama (Uelewe)
Anasa zote za dunia ni za muda
Halleluyah
Muamini Yesu Bwana wangu akuokoe
Uelewe
Yeye ni Bwana tena mueza wa yote
Halleluhya

Dunia hii isikudanganye Baba (Uelewe)
Anasa za dunia zote zinapitaga
Halleluyah
Muamini Yesu Bwana wangu akusamahe
Uelewe
Yeye ni Bwana tena mueza wa yote
Halleluhya
Tazama
Yesu kwa huruma anakubembeleza Yesu eh
Yesu yupo msalabani alisema njooni kwangu
Nitawasamehe dhambi
Nitabeba mizigo yenu
Ogopa kitimutimu
Siku yakuja kuuliwa

Yesu yupo msalabani
Anasema njooni kwangu
Nitawasamehe dhambi
Nitabeba mizigo yenu
Ogopa kitimutimu
Siku yakuja kuuliwa
Kasheeshe kwa watakaobaki kwenye viti kuu
Lyrics copyright : legal lyrics licensed by Lyricfind.
No unauthorized reproduction of lyric.

Comments for Kitimutimu lyrics

Name/Nickname
Comment
Copyright © 2004-2024 NET VADOR - All rights reserved. www.paroles-musique.com/eng/
Member login

Log in or create an account...

Forgot your password ?
OR
REGISTER
Select in the following order :
1| symbol at the bottom of the thumbs up
2| symbol at the bottom of the smiley
3| symbol to the left of the suitcase
grid grid grid
grid grid grid
grid grid grid